Aug 11, 2012


> > Jamaa
> > mmoja alikuwa akitokea shamba pamoja na mkewe. Wakiwa njiani
> > waliona uyoga, wakaung'oa na kwenda nao nyumbani kwa
> > lengo la kwenda kupika na kuula. Lakini kabla ya kufika
> > nyumbani, wakahofu kwenda kula ule uyoga wakihisi unaweza
> > kuwa si uyoga wa kula.
> > 
> > Basi wakaamua wapike uyoga kidogo,na kiasi waubakishe,
> > halafu ule waliopika wampe mbwa wao, asipokufa mbwa basi ule
> > waliobakisha nao wale. Mbwa akala uyoga ule. Wakakaa siku ya
> > kwanza,ya pili, mbwa hajafa wakaamua wapike ule uyoga
> > uliobakia nao wakala.
> > 
> > Walipomaliza kula tu, mara mtoto wao wa kiume akaingia
> > ndani akitokea shule, na kuwaeleza wazazi kuwa amemuona mbwa
> > wao amekufa.
> > 
> > Wazazi wakapigwa na butwaa wakijua basi nao mwisho wa
> > maisha yao
> > umefika, na muda wowote watakufa tu kwa kuwa nao wamekula
> > uyoga kama mbwa alivyokula.
> > Basi yule baba akaamua kumwambia mkewe anaomba atubu mbele
> > yake kwa kuwa kifo kinamjia wakati wowote. Jamaa akaanza
> > kumwambia mkewe amsamehe kwani ni maovu mengi alifanya.
> > Kwanza msichana wa kazi waliyemfukuza akiwa na ujauzito, ule
> > ni ujauzito wake. Mdogo wake na mkewe wa kike anayeishi naye
> > pale ni mpenzi wake wa siku nyingi. Pia ana watoto wengine
> > watatu nje ya ndoa, na kila mtoto ana mama yake.
> > 
> > Mama akasema nashukuru kwa hayo yote, Basi naomba nami
> > nitubu Kwako.Huyu mtoto wa kiume mdogo si wako nilizaa na
> > Shamba boy wetu na huu ujauzito nilionao sasa ni wa mpangaji
> > wetu humu ndani.
> > 
> > Jamaa kusikia hayo akapandwa na jazba ukawa ugomvi mkubwa
> > mule ndani.
> > 
> > Wakati wakigombana, mara mtoto wao wa kwanza wa kike
> > akaingia ndani na kukuta wakigombana. Akawauliza, Baba na
> > mama mnagombania nini humu ndani, badala ya kwenda kuona
> > mbwa wetu amekufa kwa
> > kugongwa na gari kule nje?
> > 
> > Wazazi waliposikia kuwa mbwa amekufa kwa kugongwa na gari
> > walibaki wanatazamana na kupigwa na bumbu wazi.
> > 
> > Fikiria ni wewe ITAKUWAJE

No comments: