Jul 29, 2013
Simu haipatikani Mama: mwanangu hebu mpigie simu baba yako mwambie chakula tayari. Mtoto: sawa mama Basi mtoto akampigia simu baba yake lakini hakumpata Mtoto: mama simpati Mama: basi subiri kama baada ya dakika tano mpigie tena inawezekana ni mambo ya network hayo.Baada ya dakika tano mtoto akampigia tena baba yake Mtoto:mama mimi baba simpati simu yenyewe anapokea mwanamke Mama: kha! sawa mwanangu niachie mimi hili suala wewe nenda kale.Baada kama ya dakika 30 baba akabisha hodi akakaribishwa na bonge la kibao hajakaa vizuri akapigwa na sufuria mara mwiko ikawa ni balaa kwa kwenda mbele mume akazidiwa mara majirani wakaja kuamulia ugomvi,lakini majirani walipofika wakakamkuta mume yuko chini ya sofa hoi bin taaban Mama: pumbavu zako we wa kunifanyia mimi hiviyaani unakwenda kwa malaya zako na kuniacha mimi hapa nyumbani? mwanangu hebu waambie majirani yule mwanamke alipo pokea simu alisemaje? Mtoto: alisema simu uliyopiga kwa sasa haipatikani jaribu tena baadae!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment