vituko na vitimbwi (Jokes)

Blog hii ni kwa ajili vijimambo vya kuchekesha na kuliwazana

Jul 29, 2013

Simu haipatikani Mama: mwanangu hebu mpigie simu baba yako mwambie chakula tayari. Mtoto: sawa mama Basi mtoto akampigia simu baba yake lakini hakumpata Mtoto: mama simpati Mama: basi subiri kama baada ya dakika tano mpigie tena inawezekana ni mambo ya network hayo.Baada ya dakika tano mtoto akampigia tena baba yake Mtoto:mama mimi baba simpati simu yenyewe anapokea mwanamke Mama: kha! sawa mwanangu niachie mimi hili suala wewe nenda kale.Baada kama ya dakika 30 baba akabisha hodi akakaribishwa na bonge la kibao hajakaa vizuri akapigwa na sufuria mara mwiko ikawa ni balaa kwa kwenda mbele mume akazidiwa mara majirani wakaja kuamulia ugomvi,lakini majirani walipofika wakakamkuta mume yuko chini ya sofa hoi bin taaban Mama: pumbavu zako we wa kunifanyia mimi hiviyaani unakwenda kwa malaya zako na kuniacha mimi hapa nyumbani? mwanangu hebu waambie majirani yule mwanamke alipo pokea simu alisemaje? Mtoto: alisema simu uliyopiga kwa sasa haipatikani jaribu tena baadae!

Posted by Willybright Elvis at 11:26 AM No comments:

Jul 28, 2013

Hata kwa ndumba maji ya moto hayaunguzi nyumba. Piga ua aliyelala chini haanguki. Kumbuka kisu nacho kinakata lakini hakina diwani. Kumbuka serikali itapandisha kila kitu ila haiwezi kupandisha mashetani. Hata dobi ajue kupiga pasi vipi hawezi kupata namba barcelona. Hata ndoa zinavunjika lakini hazifungwi P.O.P. Kumbuka umbulula ni kufuta namba ya mpenzi wako kwenye cmu wkt unaijua kichwani. Kumbuka kama mtoto mchanga basi mkubwa jiwe. Kaa ukijua umburula ni kumwandikia m2 'i lv u' na kusubiria jibu wkt cyo swali. Piga ua garagaza aliyeshinda njaa hawezi kupewa medali.

Posted by Willybright Elvis at 6:34 AM No comments:
Newer Posts Older Posts Home
Subscribe to: Posts (Atom)

Blog Archive

  • ►  2015 (1)
    • ►  January (1)
  • ►  2014 (8)
    • ►  August (1)
    • ►  June (2)
    • ►  April (2)
    • ►  March (3)
  • ▼  2013 (14)
    • ►  August (4)
    • ▼  July (2)
      • Simu haipatikani Mama: mwanangu hebu mpigie simu b...
      • Hata kwa ndumba maji ya moto hayaunguzi nyumba. Pi...
    • ►  May (2)
    • ►  April (3)
    • ►  March (1)
    • ►  January (2)
  • ►  2012 (34)
    • ►  December (3)
    • ►  September (1)
    • ►  August (13)
    • ►  July (17)
  • ►  2011 (1)
    • ►  January (1)
  • ►  2009 (10)
    • ►  February (10)
  • ►  2008 (13)
    • ►  April (3)
    • ►  March (10)

About Me

Willybright Elvis
View my complete profile
Awesome Inc. theme. Powered by Blogger.