May 23, 2013

HII INAITWA ELIMU

Jambazi: "wote laleni chini pesa ni za serikali na maisha ni ya
kwenu",wote wakalala chini.
HII INAITWA DHANA YA USHAWISHI-kubadilisha njia ya kawaida ya kufikiria
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
Kuna dada kwa woga akawa amelala chini kimitego,
Jambazi: "dada embu kuwa na adabu chukua kanga jifunike hili ni
tukio la ujambazi na sio la ubakaji. HUU UNAITWA WELEDI-zingatia ulichofundishwa kufanya
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
Walipotoka kwenye wizi jambazi mdogo ambaye ana shahada ya
uzamili ya biashara akamwambia mwenzake,"tuzihesabu hizi
fedha,yule mkubwa akamcheka kwa dharau na kumjibu,"wewe
mjinga sana hizo hazina haja ya kuhesabu saa mbili watatutangazia
kwenye taarifa ya habari tumeiba kiasi gani.

HUU INAITWA UJUZI-Sikuhizi ujuzi ndio bora kuliko vyeti
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
Baada ya majambazi kuondoka meneja akamwambia mhasibu wa
bank, " ujumlishie na zile milioni 80 tulizo iba sisi".

HUKU KUNAITWA KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI- kushabiihana na mazingira magumu kwa faida binafsi.
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
Mhasibu akafurahi na kusema,"dah wizi ukitokea kila
mwezi itakuwa burudani sana.
HUKU KUNAITWA KUWA NA MAWAZO CHANYA-Furaha ndio kitu cha muhimu zaidi
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
Meneja akafurahi sana kwa kuwa sasa matatizo yake yametatuliwa
na wizi uliojitokeza.
HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU-shikilia nafasi pale inapojitokeza hata kama ni hatari kiasi gani
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
Haya usiku wake taarifa ya habari ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana wa millioni 100 umetokea leo benki kuu,

Majambazi kusikia hivyo wakaanza kuhesabu zila pesa lakini wakajikuta na milioni 20 tu. Yule jambazi mkubwa akashtuka na kusema, "dah! yani meneja kaiba mara nne zaidi yetu bila kuchezesha msuli bora umeneja kuliko ujambazi".

HII INAITWA ELIMU- ishike sana elimu ina nguvu kuliko dhahabu

••••••••••••••••••••••••••••••••MWISHO•••••••••••••••••••••••••••

No comments: